Historia ya Nyanyuka Afrika Foundation
Nyanyuka Afrika Foundation ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa rasmi tarehe 23/05/2025 (Na. 00NGO/R/8441), likiwa na makao makuu mkoani Dodoma, Tanzania.
Kuzaliwa kwa shirika hili ni matokeo ya vuguvugu la muda mrefu la harakati za kijamii za mwanzilishi Dotto Stephen Masulubu, kuanzia mwaka 2012 kupitia klabu za wanafunzi shuleni kama vile The Bright Family Club na The Orphan Students Association (OSA). Juhudi hizi zilichanua zaidi mwaka 2019 kupitia kampeni ya mtandaoni ya "Tukomeshe Mimba Shuleni" na kufikia kilele cha uzinduzi vya kampeni kubwa ya mazingira ya "Ziara Yangu, Mti Wangu" mnamo mwaka 2024 Ilizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini.
Lengo letu kuu ni kuendelea kutoa suluhisho endelevu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, changamoto za kiuchumi, na ukosefu wa ajira kwa vijana na wanawake kupitia misingi ya mageuzi ya kifikra (mindset change) na uwezeshaji wa vitendo.
Dira (Vision)
Kuwa taasisi ya kimotisha inayoongoza nchini Tanzania kwa kusaidia wananchi kuinuka kijamii, kiuchumi na kisiasa kupitia msaada wa kihali na mabadiliko ya fikra chanya.
Dhamira (Mission)
Kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kutoa suluhisho kupitia ushirikiano na Serikali ya Tanzania, wananchi na wadau wa ndani na nje ya nchi.
Malengo Makuu (Objectives)
Kukuza maendeleo endelevu na uwezeshaji kupitia elimu, ujuzi wa kazi na ujasiriamali kwa vijana na wanawake.
Kuelimisha jamii kuhifadhi, kulinda na kusimamia rasilimali za asili na mazingira yanayotuzunguka ili kukabili mabadiliko ya tabianchi.
Kukuza utawala bora, haki za binadamu na utoaji wa elimu thabiti ya uraia kwa maendeleo ya taifa.
Kutoa msaada wa kisheria, ushauri, na elimu ya kisheria kwa makundi ya watu wasiojiweza na waliopo pembezoni mwa jamii.