Matukio
Dodoma, Tanzania — Nyanyuka Afrika Foundation imepata heshima ya kuteuliwa na kuwa miongoni mwa washiriki katika utekelezaji wa Mradi wa TACTIC, hususan katika programu ya upandaji miti na uhifadhi wa mazingira inayotarajiwa kutekelezwa katika Jiji la Dodoma. Programu hiyo inalenga kupanda miti milioni 2 ndani ya kipindi cha miaka miwili, ikiwa ni hatua muhimu katika kuongeza maeneo ya kijani, kuboresha mazingira ya Jiji la Dodoma na kuchangia juhudi za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Katika maandalizi ya utekelezaji wa programu hiyo, Nyanyuka Afrika Foundation ilishiriki TACTIC Tree Planting Programme Workshop iliyofanyika Morogoro tarehe 9–10 Julai 2026. Taasisi hiyo iliwakilishwa na Dotto Stephen Masulubu, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Nyanyuka Afrika Foundation, aliyeshiriki pamoja na wadau mbalimbali katika kujadili maandalizi na utekelezaji wa mpango huo. Mradi wa TACTIC unatekelezwa kwa uratibu wa TARURA na kufadhiliwa na Benki ya Dunia (World Bank), huku ushiriki wa Nyanyuka Afrika Foundation ukiwa sehemu ya jitihada za kuunganisha nguvu za wadau katika kulinda na kuhifadhi mazingira. Nyanyuka Afrika Foundation imeeleza kuwa inathamini nafasi hiyo na iko tayari kushirikiana na TARURA, Serikali, Benki ya Dunia, wadau wengine pamoja na jamii ya Dodoma katika kuhakikisha lengo la upandaji miti linafikiwa. 🌱 Miti Milioni 2 kwa Dodoma Leo tunapanda miti, kesho tunajenga mazingira bora kwa kizazi kijacho. NYANYUKA AFRIKA FOUNDATION Mwanga wa Kila Kizazi 🌍
Mazingira
Zoezi la ugawaji na upandaji miti limeendelea kwa mafanikio makubwa kwenye maeneo ya vyanzo vya maji.
Urithi
Uhamasishaji wa jamii kuhusu utunzaji wa urithi wa asili na ulinzi wa wanyamapori dhidi ya uharibifu.
Kukutana na kuwajengea uwezo wa kibiashara na fursa za mitandao kiuchumi wajasiriamali wadogo.
Zoezi kubwa la kupandisha miti kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji na kukabili ukame.
Cana Plaza, Dodoma | S.L.P 1249 Dodoma
+255 659 961 277 / +255 659 961 278
nyanyukaafrikafoundation@gmail.com
Kila shilingi unayochangia inakwenda moja kwa moja kununua miche ya miti, kutoa mafunzo kwa vijana, na kuimarisha mitandao ya kiuchumi ya kina mama na wafanyabiashara wadogo hapa Tanzania.