Our Core Projects
Uhifadhi wa Mazingira
Tunashughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo nchini Tanzania. Kupitia kampeni zetu za "Ziara Yangu, Mti Wangu" na "Shitaka Urithi Mazingira", tunahamasisha upandaji miti endelevu na utunzaji wa mazingira.
Msaada wa Kisheria & Uraia
Tunatoa elimu thabiti ya uraia, haki za binadamu na utawala bora. Taasisi inajikita katika kutoa msaada wa kisheria na ushauri wa bure kwa makundi ya jamii wasio na uwezo au walio katika mazingira magumu ili kuhakikisha usawa vya haki.
Uwezeshaji Kiuchumi
Kupitia mafunzo ya ujuzi wa kazi na ujasiriamali, tunalenga kuamsha fikra chanya (mindset change) kwa vijana na wanawake ili kuwawezesha kuanzisha mitandao imara ya biashara, kukuza vipato na kujenga fursa za ajira endelevu.
Maendeleo ya Jamii
Tunasimamia midahalo, makongamano na mafunzo maalum. Kupitia jukwaa letu la "Wito Wa Kunyanyuka" tunajenga jamii yenye fikra chanya na yenye kuchukua hatua za kimaendeleo kwa vitendo.